BUJUMBURA
Kampuni zinazofanya utafiti wa madini nchini Burundi, zimefurahia maboresho ya muswada wa sheria ya madini nchini humo.
Baadhi ya kampuni zimesema kwamba zimetumia nguvu nyingi na uzowefu, ili serikali ya Burundi ipate sheria ya madini inayoendana na wakati, ikizingatiwa maslahi ya nchi husika na mashirika, kama ilivyo katika nchi jirani kama Tanzania na Rwanda.
Mashirika yaho yanasema kwamba baraza la bunge na seniti nchini humo, yameonyesha uaminifu kwa mashirika hayo, na mengine yatakayo fuata hapo baadae, kama ilivyo elezewa na waziri wa nishati, madini na ardhi nchini humo.
Taarifa kutoka baadhi ya wafanyakazi wa mashirika hayo, wamefurahishwa na uamuzi wa bunge na seneti, baada ya hofu waliyokuwa nayo, kwamba mashirika hayo yangefungasha virago, na wao kupoteza ajira kwa wingi.
Wameelezea matumaini yao, kwamba na Raisi atatia saini mwasada huo, na kuwa sheria mpya ya madini, ambayo ni mkombozi wa uchumi wa nchi nyingi duniani.
Ikumbukwe kwamba sheria hiyo, itatofautisha shughuli za sekta ya madini na ile ya mafuta, ambayo itaandaliwa hapo baadaye, sheria ya madini ikisha patikana.
Hi ni website ya kukusanya habari kutoka nchini Burundi kwa kiasi kikubwa, lakini pia habari zinazohusiana na matukio mbalimbali yanayotokea katika eneo la Afrika ya Mashariki, na ulimwenguni kote kwa ujumla.
Friday, October 11, 2013
DAR ES SALAAM
Watu wawili wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya
utapeli , huku mmoja akitumia kitambulisho kinachomtambulisha kuwa ni ofisa
mwandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa, wametiwa mbaroni jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo ambalo liligusa hisia za watu wengine lilitokea juzi maeneo ya
Kawe, wakiwa katika Hoteli ya Picol Beach saa 2.30 siku baada ya kuwekewa
mtego.
Watuhumiwa hao watanashati waliokamatwa katika tukio hilo wametambuliwa
kuwa ni Fadhili Hamisi Mafutari ambaye anadaiwa kutumia kitambulisho cha Idara
ya Usalama wa Taifa, kikiwa na jina la Kennedy Magige na picha yake.
Pia anatumia simu yenye namba 0654-084-445 iliyosajiliwa kwa jina la
Kennedy Magige, ingawa rafiki yake ambaye amekamatwa naye kwenye tukio hilo,
Tabula Abdallah Mayenga, alisema anamfahamu na jina lake, Fadhili Hamisi
Mafutari.
Watu hao walikamatwa baada ya kuwekewa mtego na watu wanaodai kutapeliwa na
Mayenga katika tukio lililotokea Ijumaa, wiki iliyopita maeneo ya Maua Resort
Beach.
Akisimulia tukio hilo, mmoja wa mashuhuda alisema baada ya kutapeliwa,
walianza kuweka mtego na kufanikiwa kumnasa Magige, kwa kutumia mtu mwingine
aliyempigia simu na kujifanya ana shida naye.
Mtoa habari wetu huyo, alidai kwamba wakati Magige anawafanyia tukio hilo
la utapeli, hakuwa anafahamu k ama wamebaki na namba yake simu na baada ya
kufuatilia, walibaini imesajiliwa kwa jina la Magige.
Baada ya kufika, alitiwa mbaroni pamoja na mwenzake na kuanza kushushiwa
kipigo kikali na wananchi wenye hasira, ambapo ilibainika anamiliki
kitambulisho kinachomtambulisha kuwa ni ofisa mwandamizi Idara ya Usalama wa
Taifa.
Lakini alipohojiwa, Magige alijitambulisha kuwa yeye ni mfanyabiashara wa
mazao aina ya nafaka kauli ambayo ilitofautiana na rafiki yake ambaye
alikamatwa naye kwenye tukio hilo, kwani alisema Mafutari (Magige) ni
mfanyabiashara wa magari.
Mayenga alisema yeye ni fundi seremala na kwamba alifika hotelini hapo
kufuata hela kidogo kwa rafiki yake,lakini ghafla aliona watu wanaanza
kumfuatilia na hakuwa na njia ya kukimbia kwani alihisi ataitiwa mwizi.
Burundi: Bunge lapitisha mswada wa sheria ya madini baada ya maboresho kadhaa.
Baraza la wabunge nchini Burundi, limepitisha mswada wa sheria mpya ya madini bila kupingwa, baada ya maboresho ya sheria ya mwaka 1976.
Sheria hiyo ya zamani ilikuwa haitofautishi sekta ya madini na ile na mafuta, na kutatiza shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini.
Katika maboresho hayo, serikali ya Burundi inatakam kurahisisha shughuli nzima ya utafiti na uchimbaji, ili kampuni na watu binafsi wa nchi za nje, waweze kufanya shughuli hizo nchini humo bila matatizo.
Serikali ya Burundi itakuwa na asilimia 15 ya hisa katika kila kampuni, ili iwe rahisi kufuatilia kampuni hizo, na kuhakikisha swala la mazingira linazingatiwa.
Marekebisho mengine anahusu mikataba ya ueneshaji wa shughuli hizo, imebadirishwa, ili serikali inufaike na shughuli hizo, bila kusahau maslahi ya kampuni hizo.

Subscribe to:
Posts (Atom)