Friday, October 11, 2013

Burundi: Bunge lapitisha mswada wa sheria ya madini baada ya maboresho kadhaa.


Baraza la wabunge nchini Burundi, limepitisha mswada wa sheria mpya ya madini bila kupingwa, baada ya maboresho ya sheria ya mwaka 1976.

Sheria hiyo ya zamani ilikuwa haitofautishi sekta ya madini na ile na mafuta, na kutatiza shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini.

Katika maboresho hayo, serikali ya Burundi inatakam kurahisisha shughuli nzima ya utafiti na uchimbaji, ili kampuni na watu binafsi wa nchi za nje, waweze kufanya shughuli hizo nchini humo bila matatizo.

Serikali ya Burundi itakuwa na asilimia 15 ya hisa katika kila kampuni, ili iwe rahisi kufuatilia kampuni hizo, na kuhakikisha swala la mazingira linazingatiwa.

Marekebisho mengine anahusu mikataba ya ueneshaji wa shughuli hizo, imebadirishwa, ili serikali inufaike na shughuli hizo, bila kusahau maslahi ya kampuni hizo.


No comments:

Post a Comment