Friday, October 11, 2013

BUJUMBURA

Kampuni zinazofanya utafiti wa madini nchini Burundi, zimefurahia maboresho ya muswada wa sheria ya madini nchini humo.

Baadhi ya kampuni zimesema kwamba zimetumia nguvu nyingi na uzowefu, ili serikali ya Burundi ipate sheria ya madini inayoendana na wakati, ikizingatiwa maslahi ya nchi husika na mashirika, kama ilivyo katika nchi jirani kama Tanzania na Rwanda.

Mashirika yaho yanasema kwamba baraza la bunge na seniti nchini humo, yameonyesha uaminifu kwa mashirika hayo, na mengine yatakayo fuata hapo baadae, kama ilivyo elezewa na waziri wa nishati, madini na ardhi nchini humo.

Taarifa kutoka baadhi ya wafanyakazi wa mashirika hayo, wamefurahishwa na uamuzi wa bunge na seneti, baada ya hofu waliyokuwa nayo, kwamba mashirika hayo yangefungasha virago, na wao kupoteza ajira kwa wingi.

Wameelezea matumaini yao, kwamba na Raisi atatia saini mwasada huo, na kuwa sheria mpya ya madini, ambayo ni mkombozi wa uchumi wa nchi nyingi duniani.

Ikumbukwe kwamba sheria hiyo, itatofautisha shughuli za sekta ya madini na ile ya mafuta, ambayo itaandaliwa hapo baadaye, sheria ya madini ikisha patikana.

No comments:

Post a Comment